Donald Trump ataka mabadiliko katika udhibiti wa silaha Marekani

0
175

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine, amelaani mauaji ya zaidi ya watu 30 baada ya matukio mawili ya watu kupipgwa risasi nchini humo, mwishoni mwa wiki iliyopita

Trump amesema kuwa, kinachotokea kinaonesha kiwango cha chuki na ubaguzi nchini humo, lakini pia amelaani kile alichokieleza kuwa Wamarekani wazungu kuona kuwa wana mamlaka zaidi, suala ambalo amesema halikubaliki katika taifa hilo wakati huu nchi hiyo inapoendelea na jitihada za kupambana na matumizi mabaya ya silaha.

Rais Donald Trump ameyaelezea mashambulizi katika majimbo ya Texas na Ohio kuwa ni uhalifu dhidi ya taifa na dhidi ubinaadamu.

Jumla ya watu zaidi ya 31 wameuawa katika mashambulio ya bubduki kwenye majimbo ya Texas na Ohio mwishoni mwa wiki.

Watu 20 waliuawa kwa kupigwa risasi wakati wakifanya manunuzi kwenye duka la Walmart katika mji wa El Paso siku ya Jumamosi na wengine tisa katika eneo la Dayton masaa 13 tu baadaye.

Wakati huo huo rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amewataka Wamarekani kukataa lugha za chuki na kibaguzi kutoka kwa viongozi wao.

Mapema Trump alitoa mwito kwa wabunge kupitisha sheria kali ya kuchunguza wanunuzi ya silaha kufuatia mashambulizi hayo mabaya ingawa pia alitaka mabadiliko hayo yaendane na sera ya wahamiaji.

Pamoja na RFI

 

ACHA JIBU

Please enter your comment!
Please enter your name here