Misri :Rais wa zamani Mohamed Morsi afariki mahakamani.

0
91

Televisheni ya Taifa ya Misri imeripoti Rais wa zamani Mohamed Morsi alianguka mahakamani na kuaga dunia.Kituo hicho kimesema rais huyo wa Misri aliyepinduliwa mwenye umri wa miaka 67 alikuwa amefikishwa mahakamani Jumatatu kusikiliza kesi yake juu ya mashtaka ya ujasusi ambapo alianguka. Kituo cha televisheni alifariki kabla ya kupelekwa hospitali.

Morsi, kiongozi wa juu wa Kikundi cha Muslim Brotherhood, alipinduliwa akiwa katika wadhifa wa urais na Jeshi la Misri baada ya maandamano makubwa dhidi ya uongozi wake.

Kikundi cha Muslim Brotherhood baada ya hapo kilipigwa marufuku na jeshi na Morsi alikamatwa. Rais huyo wa zamani alikuwa anatumikia kifungo cha miaka saba kwa kughushi ombi lake la kugombea urais mwaka 2012 na alikuwa anakabiliwa na mashtaka mengine ya ujasusi.

Kikundi cha haki za binadamu cha Human Rights Watch kimeeleza kuwa mashtaka dhidi ya Morsi ni ya kisiasa. Mkurugenzi Mtendaji wa kikundi hicho Mashariki ya Kati, Sarah Leah Whitson, alituma ujumbe wa tweet Jumatatu akisema kufungwa kwa Morsi ni “ukatili na kinyume cha ubinadamu” ikiwemo kunyimwa haki ya kutembelewa na familia yake na huduma za afya.”

Morsi alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012 katika uchaguzi huru wa kwanza Misri baada ya kiongozi wa muda mrefu wa zamani Hosni Mubarak kuondolewa madarakani.

Pamoja na BBC Afrika

ACHA JIBU

Please enter your comment!
Please enter your name here